Pages

Thursday, March 7, 2019

DALILI ZA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE




Dalili za ugonjwa wa vidonda vya tumbo

Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni kuchoka choka sana bila sababu maalum, kuuma mgongo au kiuno, kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia, kizunguzungu, kukosa usingizi, usingizi wa mara kwa mara. Maumivu makali sehemu ya mwili, kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali.

Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali. Dalili zingine ni kichefuchefu, kiungulia, tumbo kujaa gesi, tumbo kuwaka moto, maumivu makali sehemu kilipo kidonda, kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi.

Kutapika nyongo, kutapika damu au kuharisha, sehemu za mwili kupata ganzi n.k. Pia dalili zingine ni kukosa hamu ya kula, kula kupita kiasi, kusahahu sahau na hasira. Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.

Vidonda vya tumbo husababishwa na nini?

Linapokuja suala la nini husababisha vidonda vya tumbo unaweza ukapata stori nyingi bila idadi, lakini kwa kifupi kabisa; vidonda vya tumbo ni ishara za mwili kupungukiwa maji na kama matokeo ya asidi kuzidi mwilini kuliko alkaline. Vinaweza pia kuletwa na bakteria ajulikanaye kama H.Pyroli.

Vidonda via Tumbo vinatibika
Kwa kuwa asidi inavyozidi mwilini husababisha vidonda vay Tumbo na kuzaliwa kwa bacteria aina ya H.PYROL 

Splina Liquid chlorophyll imekuwa ni suluhisho la Ugonjwa huu na kuwasaidia watu wengi kwa sababu zifuatazo:

  • inasaidia kubalance asidi kuwa alkaline 
  • inamadini mengi ya zinc na magnesium ambayo yanasaidia vidonda kupona kwa haraka
  • inasaidia pia kuuwa bacteria aliyepo kwenye kidonda na kuzuia asiendelee kushambulia 
  • inamadini mengi ambayo mwili unahitaji
  • inaondoka gas tumboni
  • inarekebisha mmengenyo wa chakula tumboni
Kwa maelezo zaidi na kwa mahitaji ya dawa za vidonda vya tumbo, gas kiungulia wasiliana nasi kwa 0758768855


Wednesday, February 27, 2019

Tatizo la kukosa Choo na tiba yake





Je!Unatatizo la Kukosa Choo?
Mtu yeyote ambaye anapata walau mlo mmoja kwa siku na kupitisha kati ya siku moja au tatu bila kupata choo, ana tatizo la kukosa choo (Constipation).

NINI KINASABABISHA KUKOSA CHOO?
· Kukosa mlo kamili. Kama vile kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha wanga na mafuta.
· Kula vyakula vilivyokobolewa na vilivyo changanywa na madawa ili visiharibike.
· Mifumo hatarishi ya maisha kama vile matumizi ya sigara na pombe uliokithiri.
· Ukosefu wa kiwango cha kutosha cha mbogamboga na matunda katika mlo, ila nakushauri ule matunda saa moja au mbili kabla ya mlo au saa moja au mbili baada ya mlo.
· Maji yasiyo salama.
· Kuvuta hewa chafu.
· Na nyingine nyingi zinazosababishwa na maisha yanayoendeshwa na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

ATHARI ZA KUKOSA CHOO
· Chakula kutomeng’enywa (kusagwa) vizuri.
· Maumivu makali wakati wa kupata choo.
· Uchafu uliokaa kwa muda mrefu kugeuka sumu.
· Bakteria wenye madhara kuzaliwa na kuathiri utumbo mpana na viungo vingine mwilini.

NI MAGONJWA GANI SUGU YANAYOWEZA KUSABABISHWA?
· Saratani ya utumbo mpana (colon cancer)
· Presha
· Kuongeza uzito (obesity)
· Tumbo kujaa gesi
· Magonjwa ya ini
· Figo kushindwa kufanya kazi vizuri
· Maginjwa ya ngozi
· Kukakamaa kwa mishipa ya damu
· Kisukari
· Magonjwa ya moyo
· Na matatizo mengine mengi

NI NINI SULUHISHO SAHIHI LA TATIZO LA KUKOSA CHOO?
Ondoa mgandamano wote wa taka katika utumbo mpana ukiuacha ikiwa msafi na wenye afya zaidi.
FAIDA YA KUONDOA MGANDAMANO
· Ni njia haraka na salama kwa afya yako
· Inazuia saratani ya utumbo mpana (colon cancer) na madhara mengine kiafya (coprostasis)
· Tatizo la kukosa choo utakuwa umelimaliza
· Utapunguza uzito uliozidi
· Utaifanya ngozi iwe yenye afya, nyororo na muonekano mzuri
Samahani kwa kusema hivi, lakini ni ukweli uliowazi kuwa watanzania tuna aibu sana ya kuingia maliwato huku tunaangaliwa na watu wengine. Hii ni mbaya sana kwa kuwa pale unapobana haja kubwa ukasema nitaenda baadaye unatengeneza pochi katika utumbo, chunguza mara ngapi umejibana kuanzia wakati huo hadi umri huo ulio nao, ni vipochi vingapi umetengeneza, una takataka kiasi gani katika utumbo mpana?
Utafanya mazoezi, utapunguza kula utakunywa baadhi ya dawa za kupunguza mafuta mwilini lakini utabaki na kitambi kikubwa unajua kwanini? Kwa sababu ya vipochi ulivyovitengeneza kwa kubana choo.
Pili hata ukiingia maliwato unakimbiakimbia likitoka tonge moja basi umeshanawa umekimbia, ni hatari sana kufanya hivyo, unatakiwa ukae kuanzia dakika 10 na kuendelea ili kila kilichokuwa kinatakiwa kutoka kitoke kwa wakati huo.
Tatu, usilazimishe au usijikamue ili kutoa unachohisi kipo unachotakiwa kufanya hakikisha umejiachia na kuiacha misuli ijifungue yenyewe kwa wastani wake ili kilichopo kitoke kama kinavyotakiwa. Ikilazimisha ndio yale yale kubakiza vipochi kila siku.
Kwa kweli wengi wetu tunakosea mambo mengi sana katika maisha yetu, kuanzia kula, kulala, kuvaa, kujisaidia haya yote ukifuatilia utakuta tunajitengenezea magonjwa bila kujua.
JE UTAJUA KUWA RANGI YA KINYESI, HARUFU YA KINYESI VINAWEZA KUKUONESHA UNA UGONJWA GANI AU BAKTERIA KIWANGO GANI?
JE UNAJUA KUWA MUUNDO AU SHAPE YA KINYESI INAWEZA KUKUTAMBULISHA UNA SHIDA GANI
· Kama kinyesi chako ni kama ndizi uko sawa
· Kama kinyesi chako ni kama mbuzimbuzi kuna shida aidha ya maji hunywi ya kutosha
· Kama kinyesi kina tawanyika kama mafuta kuna shida
· Kikiwa hakina shape pia ni shida
· Kinyesi kikiwa kinashika katika sinki la choo ni shida kubwa sana hiyo pia
· Kinyesi kikiwa na harufu mbaya kali ni tatizo kubwa pia
Hili ni somo nalo tutalisoma kwa kifupi naomba uendelee kuwa nami.
Kama utaona una matatizo au tatizo lolote katika haya niliyotaja hapa, hasa kukosa choo, vidonda vya tumbo, gesi tumboni, manyama uzembe, matatizo ya ngozi, basi wasiliana nami
ili tujue la kufanya.

Kwamaelezo zaidi wasiliana
whatsapp/call +255758768855, +255716768855

Tuesday, February 19, 2019

Ugonjwa wa Goita na Tiba yake



Goita (Goiter) ni hali ya kuvimba kwa tezi ya thyroid. Uvimbe huu hautokani na saratani na kwamba goita si saratani. Tezi ya thyroid ipo sehemu ya mbele ya shingo. Kazi kuu za tezi ya thyroid ni kuzalisha homoni mbalimbali ambazo husaidia mwili kuthibiti na kufanya kazi zake mbalimbali.
Aina za goita na visababishi vyake
Kuna aina kadhaa za goita. Goita ya kawaida (simple goiter) inaweza kutokea bila kuwepo kwa chanzo chochote cha kueleweka. Wakati mwingine, yaweza kutokea wakati tezi ya thyroid inaposhindwa kuzalisha homoni/vichocheo vya kutosha vya thyroid kwa ajili ya mahitaji ya mwili. Ili kuweza kuendana na hali hii, tezi ya thyroid huongezeka ukubwa ili kufidia upungufu wa homoni za thyroid.
Kuna aina mbili za goita ya kawaida, Goita inayowapata wakazi wa eneo fulani (endemic goiter). Aina hii pia huitwa colloid goiter, na Goita inayotokea maeneo tofauti (sporadic goiter). Aina hii pia hujulikana kama nontoxic goiter.
Endemic goiter au colloid goiter huwapata makundi ya watu wanaoishi maeneo yenye udongo wenye upungufu mkubwa wa madini ya Iodine. Maeneo ya aina hii mara nyingi ni yale yaliyo mbali kutoka pwani ya bahari au yaliyo katika nyanda za juu kutoka usawa wa bahari kama vile mikoa ya Mbeya, Iringa na Rukwa. 
Iodine ni madini muhimu yanayohitajika katika utengenezaji wa homoni mbalimbali zinazozalishwa na tezi ya thyroid. Watu wanaoishi kwenye maeneo kama haya wapo katika hatari ya kupata goita kwa vile hawapati madini ya kutosha ya Iodine katika chakula chao.
Matumizi ya chumvi ziliongezwa madini ya Iodine yamesaidia sana kupunguza matatizo ya upungufu wa Iodine miongoni mwa watu wengi nchini Tanzania na duniani kwa ujumla. Hata hivyo, upungufu wa madini ya Iodine bado umeendelea kuzikumba sehemu nyingi za Afrika ya kati, Amerika ya kusini pamoja na Asia ya kati.
Chanzo cha sporadic goiter au nontoxic goiter bado hakifahamiki vema miongoni mwa wagonjwa wengi. Hata hivyo, matumizi ya baadhi ya dawa kama vile lithium pamoja na aminoglutethimide yameelezwa kuwa chanzo kimojawapo cha aina hii ya goita.
Vihatarishi vya goita
Kuna baadhi ya mambo yanayohusiana na kurithi yanayoweza kusababisha mtu kupata goita. Vihatarishi hivi ni pamoja na:
•    Kuwa na umri kuanzia miaka 40 na kuendelea
•    Historia ya ugonjwa wa goita miongoni mwa wanafamilia
•    Hali ya kuwa mwanamke
•    Na, kutopata iodine ya kutosha katika lishe
Dalili za goita
Dalili kuu ya goita ni kuvimba au kuongezeka ukubwa kwa tezi ya thyroid. Ukubwa wa tezi unaweza kuwa kijiuvimbe kidogo katika tezi au uvimbe mkubwa kama nundu sehemu ya mbele ya shingo. Kuvimba kwa tezi ya thyroid kunaweza kusababisha mgandamizo katika njia ya hewa na mrija wa chakula, hali ambayo inaweza kusababisha:
•    Shida katika kupumua
•    Kikohozi
•    Sauti kuwa ya mikwaruzo
•    Shida wakati wa kumeza chakula 
•    Wakati mwingine, mishipa ya damu ya shingoni inaweza kuvimba pia na kusababisha mtu kujihisi kizunguzungu pindi anapoinua mikono yake juu
Uchunguzi na vipimo
Ili kuweza kutambua iwapo mgonjwa ana uvimbe kwenye tezi ya thyroid, daktari huchunguza shingo ya mgonjwa pindi anapojaribu kumeza mate yake ili kuona kama kuna uvimbe unaopanda na kushuka wakati mgonjwa anapojaribu kumeza. Daktari pia hupapasa sehemu za mbele za shingo ili kuchunguza iwapo kuna uvimbe wowote maeneo hayo.
Vipimo ni pamoja na:
•    Kupima kiwango cha homoni ya thyroxine (free thyroxine fT4)
•    Kupima kiwango cha homoni inayochochea tezi ya thyroid kuzalisha homoni nyingine yaani Thyroid stimulating hormone (TSH)
•    Ultrasound ya tezi ya thyroid. Ikiwa vivimbe (nodules) vitaonekana wakati wa kufanya ultrasound, mgonjwa hana budi kufanyiwa biopsy (kukata sehemu ya vivimbe hivyo) kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara ili kujiridhisha kuwa mgonjwa hana matatizo ya saratani ya thyroid.
•    Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa uchunguzi wa tezi ya thyroid kwa kutumia  teknolojia ya mionzi ya nuklia yaani thyroid scan ambayo, pamoja na mambo mengine husaidia kuonesha jinsi tezi ya thyroid inavyofanya kazi (thyroid uptake)
Matibabu
Goita huitaji matibabu iwapo tu inasababisha dalili zinazomletea mgonjwa usumbufu. Matibabu ya goita hujumuisha:
  • Matumizi ya madini ya mionzi ya iodine (radioactive iodine) yaani I-131 kwa ajili ya kupunguza ukubwa wa tezi ya thyroid hususani iwapo tezi hiyo inazalisha kiasi kikubwa cha homoni
  • Upasuaji wa kuondoa tezi yote yaani (total thyrodectomy) au kuondoa sehemu ya tezi (partial thyrodectomy)
  • Iwapo goita inasababishwa na upungufu wa madini ya Iodine, mgonjwa anaweza kupewa kiasi kidogo cha dawa ya maji aina ya Lugol's iodine au mchanganyiko wa potassium iodine
  • Iwapo goita inasababishwa na tezi ya thyroid inayofanya kazi chini ya uwezo wake, mgonjwa anaweza kupewa homoni za thyroid ili kufidia upungufu wowote
  • Matumizi ya dawa lishe yeye mchanganyiko wa Splina liquid chlorophyll, shake off phyto fiber, Hawaii spirulina na cafe 73 yanasaidia sana mwili kuzalisha hormone za thyroid na kuupa miili madini muhimu kama iodine na madini muhimu katika mwili 


Matarajio

Goita ya kawaida inaweza kuisha yenyewe au inaweza kuendelea kuongezeka ukubwa mpaka kumsababishia mgonjwa usumbufu. Kadiri uharibifu wa tezi ya thyroid unavyoendelea, hufikia wakati tezi hii huacha kabisa kutengeneza homoni hali inayoitwa kwa kitaalamu hypothyroidism. Mara chache, goita inaweza kubadilika na kuanza kuzalisha homoni za thyroid bila kuchochewa na kitu chochote. Hali husababisha kuwepo kwa kiasi kikubwa cha homoni za thyroid, hali inayoitwa kitaalamu kama hyperthyroidism.

Madhara ya goita
•    Shida wakati wa kumeza au kupumua
•    Kiwango cha chini cha homoni za thyroid (Hypothyroidism)
•    Kiwango cha juu cha homoni za thyroid (Hyperthyroidism)
•    Saratani ya tezi ya thyroid (thyroid cancer)
•    Goita yenye vivimbe inayozalisha homoni kwa wingi (toxic nodular goiter)
Kinga
Matumizi ya chumvi ya mezani iliyowekwa madini ya iodine husaidia kuzuia uwezekano wa kupata goita. Aidha inashauriwa kumuona daktari au mtaalamu wa afya pindi unapoona kuna uvimbe wowote sehemu za mbele za shingo.

Kwa maelezo zaidi juu ya tiba ya Goita 
wasiliana nasi 0758768855 au 0716768855