Pages

Wednesday, February 27, 2019

Tatizo la kukosa Choo na tiba yake





Je!Unatatizo la Kukosa Choo?
Mtu yeyote ambaye anapata walau mlo mmoja kwa siku na kupitisha kati ya siku moja au tatu bila kupata choo, ana tatizo la kukosa choo (Constipation).

NINI KINASABABISHA KUKOSA CHOO?
· Kukosa mlo kamili. Kama vile kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha wanga na mafuta.
· Kula vyakula vilivyokobolewa na vilivyo changanywa na madawa ili visiharibike.
· Mifumo hatarishi ya maisha kama vile matumizi ya sigara na pombe uliokithiri.
· Ukosefu wa kiwango cha kutosha cha mbogamboga na matunda katika mlo, ila nakushauri ule matunda saa moja au mbili kabla ya mlo au saa moja au mbili baada ya mlo.
· Maji yasiyo salama.
· Kuvuta hewa chafu.
· Na nyingine nyingi zinazosababishwa na maisha yanayoendeshwa na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

ATHARI ZA KUKOSA CHOO
· Chakula kutomeng’enywa (kusagwa) vizuri.
· Maumivu makali wakati wa kupata choo.
· Uchafu uliokaa kwa muda mrefu kugeuka sumu.
· Bakteria wenye madhara kuzaliwa na kuathiri utumbo mpana na viungo vingine mwilini.

NI MAGONJWA GANI SUGU YANAYOWEZA KUSABABISHWA?
· Saratani ya utumbo mpana (colon cancer)
· Presha
· Kuongeza uzito (obesity)
· Tumbo kujaa gesi
· Magonjwa ya ini
· Figo kushindwa kufanya kazi vizuri
· Maginjwa ya ngozi
· Kukakamaa kwa mishipa ya damu
· Kisukari
· Magonjwa ya moyo
· Na matatizo mengine mengi

NI NINI SULUHISHO SAHIHI LA TATIZO LA KUKOSA CHOO?
Ondoa mgandamano wote wa taka katika utumbo mpana ukiuacha ikiwa msafi na wenye afya zaidi.
FAIDA YA KUONDOA MGANDAMANO
· Ni njia haraka na salama kwa afya yako
· Inazuia saratani ya utumbo mpana (colon cancer) na madhara mengine kiafya (coprostasis)
· Tatizo la kukosa choo utakuwa umelimaliza
· Utapunguza uzito uliozidi
· Utaifanya ngozi iwe yenye afya, nyororo na muonekano mzuri
Samahani kwa kusema hivi, lakini ni ukweli uliowazi kuwa watanzania tuna aibu sana ya kuingia maliwato huku tunaangaliwa na watu wengine. Hii ni mbaya sana kwa kuwa pale unapobana haja kubwa ukasema nitaenda baadaye unatengeneza pochi katika utumbo, chunguza mara ngapi umejibana kuanzia wakati huo hadi umri huo ulio nao, ni vipochi vingapi umetengeneza, una takataka kiasi gani katika utumbo mpana?
Utafanya mazoezi, utapunguza kula utakunywa baadhi ya dawa za kupunguza mafuta mwilini lakini utabaki na kitambi kikubwa unajua kwanini? Kwa sababu ya vipochi ulivyovitengeneza kwa kubana choo.
Pili hata ukiingia maliwato unakimbiakimbia likitoka tonge moja basi umeshanawa umekimbia, ni hatari sana kufanya hivyo, unatakiwa ukae kuanzia dakika 10 na kuendelea ili kila kilichokuwa kinatakiwa kutoka kitoke kwa wakati huo.
Tatu, usilazimishe au usijikamue ili kutoa unachohisi kipo unachotakiwa kufanya hakikisha umejiachia na kuiacha misuli ijifungue yenyewe kwa wastani wake ili kilichopo kitoke kama kinavyotakiwa. Ikilazimisha ndio yale yale kubakiza vipochi kila siku.
Kwa kweli wengi wetu tunakosea mambo mengi sana katika maisha yetu, kuanzia kula, kulala, kuvaa, kujisaidia haya yote ukifuatilia utakuta tunajitengenezea magonjwa bila kujua.
JE UTAJUA KUWA RANGI YA KINYESI, HARUFU YA KINYESI VINAWEZA KUKUONESHA UNA UGONJWA GANI AU BAKTERIA KIWANGO GANI?
JE UNAJUA KUWA MUUNDO AU SHAPE YA KINYESI INAWEZA KUKUTAMBULISHA UNA SHIDA GANI
· Kama kinyesi chako ni kama ndizi uko sawa
· Kama kinyesi chako ni kama mbuzimbuzi kuna shida aidha ya maji hunywi ya kutosha
· Kama kinyesi kina tawanyika kama mafuta kuna shida
· Kikiwa hakina shape pia ni shida
· Kinyesi kikiwa kinashika katika sinki la choo ni shida kubwa sana hiyo pia
· Kinyesi kikiwa na harufu mbaya kali ni tatizo kubwa pia
Hili ni somo nalo tutalisoma kwa kifupi naomba uendelee kuwa nami.
Kama utaona una matatizo au tatizo lolote katika haya niliyotaja hapa, hasa kukosa choo, vidonda vya tumbo, gesi tumboni, manyama uzembe, matatizo ya ngozi, basi wasiliana nami
ili tujue la kufanya.

Kwamaelezo zaidi wasiliana
whatsapp/call +255758768855, +255716768855

No comments:

Post a Comment